SvenskaMSITU WA MVUA NI NINI?

Kila msitu wa mvua ni tofauti lakini kuna mambo fulani ambaye inapatikana kwa kila msitu ya mvua.
  1. Mahali Misitu ya mvua inapatikana kwa eneo ya jua �tropiki�
  2. Mvua: misitu ya mvua inapata angalau inchi 80 za mvua kila mwaka
  3. Mwavuli: misitu ya mvua ina mwavuli ambaye ni safu ya matawi na majani inayotengezwa na miti ya msitu wa mvua inayopatana karibu. Karibu mimea na wanyama wote wa msitu wa mvua wanaishi kwa mwavuli. Mwavuli inaweza kuwa futi 100 kutoka chini.
  4. Mazingira tofauti: misitu ya mvua ina kiwango kikubwa cha utofauti wa biolojia au mazingira tofuati Biodiversity au utafauti wa biolojia ni jina ya viumbo vyote ambacho ziko hai � mimea, wanyama na uyoga � inayopatikana kwa mazingira. Wanasayansi wanaamini kwamba karibu nusu ya mimea na wanyama inayopatikana kwa ardhi ya dunia inaishi kwa misitu ya mvua
  5. Hali ya utengemeano kati ya viumbo: Viumbo ndani ya msitu wa mvua mara nyingi ufanya kazi pamoja. Uhusiano wa utengemeano ni uhusiano ambayo viumbo viwili zinafaidika kwa kusaidiana. Kwa mfano mimea nyingine zinatengezea wadudu miundo ya mazingira na sukari. Hawa wadudu nawo wanalinda mimea hii kutoka kwa wadudu wengine wangeotaka kukula majani yao.

Na Rhett A. Butler
Home | Kila Kitu Kuhusu | English | PDF

�2007 Rhett Butler