Svenska
Le for�t humide


MWAVULI NI NINI?

Kwa msitu wa mvua karibu mimea na wanyama wote hawapatikani kwa sakafu ya msitu mbali wanapatikana dunia ya majani inayojulikana kama mwavuli. Mwavuli ambayo inaweza kuwa futi 100 juu ya ardhi inatengezwa na mchanganyiko wa matawi na majani ya miti ya msitu wa mvua. Wasayansi wanakadiria kwamba asilimia 70-90 ya maisha ya msitu wa mvua inapatikana kwa miti, na ifanya hii iwe mazingira kubwa zaidi ya mimea na wanyama. Wanyama wengi wanayojulikana kama tumbili, chura, vijusi, ndege, nyoka na paka ndogo zinapatikana kwa mwavuli.

Mazingira ya mwavuli ni tofauti sana na mazingira ya sakafu ya msitu Mchana, mwavuli inakuwanga imekauka nainakuwa na joto kushinda sehemu zingine za msitu na mimea na wanyama wanayoishi huko wamezoeya hii maisha ya miti. Kwa mfano kwa sababu kiwango ya majani kwa mwavuli inaifanya ngumu kuona mbele ya futi chache, wanyama wengi wa mwavuli wanatengemea mwito wa sauti kubwa au nyimbo kwa uwasiliano. Vipengo kati ya miti inaimaanisha kwamba wanyama wengine wa mwavuli wanaruka au wanaenea juu ya miti.

Wanasayansi kwa muda mrefu wamekuwa wakitaka kuchunguza mwavuli lakini kwa sababu ya urefu wa miti ya misitu ya mvua utafiti mpaka hivi karibuni umekuwa shida. Siku hizi kuna mahali maalum zinayo na daraja za kamba, ngazi na minara kusaidia wanasayansi kuzumbua siri za mwavuli.

Mwavuli ni moja tu wa safu za wima kadhaa ndani ya msitu wa mvua. Anghalia diagram upande wa ushoto kuona mipangilio nyengine ( overstory, understory, mpangilio wa kichaka na sakafu ya msitu).
Na Rhett A. Butler
Home | Kila Kitu Kuhusu | English | PDF

�2007 Rhett Butler