Svenska



KWA NINI MISITU YA MVUA INA AINA NYINGI YA MIMEA NA WANYAMA?

Misitu ya mvua ya tropiki inalisha aina kubwa zaidi ya viumbo venye hai duniani. Licha ya kuchukuwa chini ya asilimia 2 ya ukumbwa ya ardhi ya dunia misitu ya mvua iko na juu ya asilimia 50 ya mimea na wanyama duniani. Hapa kuna mfano wa utajiri wa misitu ya mvua:
  • misitu ya mvua ina aina ya 170,000 ya mimea 250,000 ya dunia ambayo inajulikana
  • Marekani ina aina ya chura 81 naye Madagascar ambaye ni ndogo kushinda Texas ina aina 300.
  • Europa ina aina ya vipepeo 321 nayo mbuga wa msitu wa mvua wa Peru (Mbuga wa Taifa wa Manu) una aina 1300.
Misitu ya mvua ina mimea na wanyama wengi kwa sababu zifuatayo:
  • Hewa: kwa sababu misitu ya mvua inapatikana kwa eneo ya tropiki ina pata jua nyingi. Hii jua inabadilishwa kuwa kawi na mimea ikitumia njia ya usanidinuru. Kwa sababu kuna jua nyingi hii inaimaanisha kuwa kawi nyingi kwa msitu wa mvua. Hii kawi inawekwa kwa mimea inayokulwa na wanyama. Kwa sababu kuna chakula nyingi kuna aina nyingi ya mimea na wanyama.
  • Mwavuli: hali ya mwavuli inaimaanisha kuna sehemu nyingi ya mimea kukuwa na wanyama kuishi. Mwavuli inapeyana njia mpya ya chakula, malazo, na mahali ya kujifisha na inapeyana pahali pengine pa viumbo mbali mbali kuathiriana. Kwa mfano kuna mimea kwa jina bromeliads ambayo inahifadhi maji kwa majani yake. Wanyama kama chura wanatumia mifuko wa maji kwa kuwinda na kutaga mayai.





Na Rhett A. Butler




Home | Kila Kitu Kuhusu | English | PDF

�2007 Rhett Butler